Kiswahili

Je, unahitaji msaada kulipia gharama za huduma zako?

Ikiwa hujaweza kulipia gharama zako za umeme, gesi ya asili au maji katika kipindi cha janga la COVID-19, msaada unapatikana.

Pigia simu kampuni yako ya huduma. Uliza maswali haya mawili:

  • Ni programu gani za msaada unazostahili kupokea?
  • Je, mnaweza kuanzisha mpango wa malipo kwa deni lako lililopita?

Je, unahitaji msaada kuwasiliana na huduma zako za umeme, gesi ya asili au maji? Andika anwani yako katika ramani iliyo katika ukurasa huu: https://www.commerce.wa.gov/utility-assistance/.

Huenda ukastahili kuwa katika programu ya serikali inayosaidia watu kulipia gharama za huduma.

Ikitegemea mapato yako, huenda ukastahili kuwa katika programu ya shirikisho inayoitwa “LIHEAP” (programu ya msaada wa nishati ya nyumbani kwa wenye mapato madogo). Programu mpya, sawia na hio kwa ajili ya gharama za maji inatengenezwa. Hii ni mifano michache ya viwango vya mapato vinavyostahili:

  • Familia ya mtu 1 = mapato ni chini ya dola 1,595 kwa mwezi au dola 19,140 kwa mwaka
  • Familia ya watu 2 = mapato ni chini ya dola 2,155 kwa mwezi au dola 26,860 kwa mwaka
  • Familia ya watu 4 = mapato ni chini ya dola 3,275 kwa mwezi au dola 39,300 kwa mwaka

Kwa habari, piga 2-1-1 au pigia “shirika la utendaji katika jamii” ya kienyeji mahali unapoishi. Tumia ramani hii kupata anwani: https://fortress.wa.gov/com/liheappublic/Map.aspx

Rasilimali zinapatikana ili kusaidia na gharama nyinginezo. Piga 2 1-1 kwa habari.

Janga hili limewaacha watu wengi Washington na gharama zisizotazamiwa. Hauko peke yako. Piga 2-1-1 ili kuzungumza na mtu anayeweza kukuunganisha na programu zinazosaidia watu kulipia vitu kama kodi, chakula, intaneti yenye uwezo mkubwa na zaidi.

Last Updated 2021-06